Meneja wa Manchester
United Louis van Gaal ameilazimisha PSG kulipa pauni milioni 3 za ziada
kwa ajili ya kumsajili Angel Di Maria, 27, baada ya mchezaji huyo
kuonekana akiwa na mmiliki wa PSG nchini Qatar (Daily Mirror),
Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa 28 kutoka
Barcelona kwa pauni milioni 20 (Sun), Van Gaal katika kumshawishi Pedro
amesema atampa nafasi katika safu ya ushambuliaji kushirikiana na Wayne
Rooney na Memphis Depay (Daily
Telegraph), Sunderland wanazungumza na Manchester United kuhusu
kumsajili kwa mkopo Adnan Januzaj, 20 (Sunderland Echo), meneja wa
Manchester United Louis van Gaal yuko tayari kumuanzisha kipa Sergio
Romero weekend hii na kutomchezesha David De Gea (daily Star), Wolfsburg
wapo tayari kumuuza kiungo wao Kevin De Bryne, 24 kwenda Manchester
City lakini kwa pauni milioni 50 (Daily Mirror), wakala wa beki wa
Augsburg, Baba Rahman, 21 anasema beki huyo wa kushoto anakaribia
kusajiliwa na Chelsea baada ya kukubaliana maslahi binafsi (Daily Star),
Chelsea pamoja na Juventus wamezungumza na Calgiari kuhusiana na
kumsajili kiungo kutoka Ghana Godfred Donsah, 19 (Daily Express), West
Brom wamejitokeza kumsajili kiungo wa Anderlecht Dennis Praet, 21
anayesakwa pia na Arsenal (Talksport), West Brom wameambiwa lazima watoe
pauni milioni 10 kumpata winga wa QPR Matt Phillips, 23 (The Sun), West
Ham wapo tayari kurejea Manchester United na kitita cha pauni milioni
12 kumtaka mshambuliaji Javier Hernandez (London Evening Standard),
Chicharito pia ataomba bei yake ya pauni milioni 12 kupunguzwa, huku
Tottenham pia wakimtaka (Daily Star), Liverpool huenda wakakamilisha
usajili wa Alexandre Lacazette, 24, baada ya klabu yake ya Lyon
kumwambia mshambuliaji huyo kuwa anaweza kuondoka (L'Equippe), Everton
wana wasiwasi wa kumpoteza beki wao John Stones, 21, baada ya Chelsea
kutayarisha dau la tatu la pauni milioni 30 (Daily Telegraph), Kevin
Prince Boateng amewasili mjini Lisbon tayari kusaini mkataba wa miaka
miwili na Sporting Lisbon (A Bola) na Crystal Palace wamemsajili winga kutoka Mali, Bacary Sako, 27 kwa mkataba wa miaka mitatu Share tetesi hizi na wapenda soka
wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!!
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment