Mkwaju wa penalti uliofungwa na
nahodha Wayne Rooney uliisaidia Manchester United kuichapa Sunderland
mabao 2-0 baada ya West Brown kupewa kadi nyekundu katika kile
kilichoonekana kama maonevu.
Rooney alifunga baada ya mshambuliaji
Radamel Falcao kuchezewa visivyo na kusababisha kutolewa kwa Wes Brown
badala ya John Oshea aliyecheza vibaya licha ya pingamizi kutoka kwa
mashabiki.Manchester united iliongeza bao la pili baada ya Rooney kufunga kupitia kichwa baada ya mkwaju wa Adnan Januzaj kupanguliwa na kipa.
Ushindi huo umeimarisha harakati za kilabu hiyo kuwania nafasi nne bora katika ligi hiyo.
Matokeo mengine:
West Ham 1 - 3 Crystal Palace
Burnley 0 - 1 swansea
Newcastle 1 - 0 Aston Villa
Stoke 1 - 0 Hull
West Brom 1 - 0 Southampton
0 comments:
Post a Comment