Tume ya uchaguzi nchini Tanzania
imesogeza mbele kwa wiki moja zaidi tarehe ya kuzinduliwa kwa zoezi la
daftari la wapiga kura litakalotumia mfumo mpya wa kieletroniki yaani
Biometric Voters Registration BVR. Zoezi hilo ambalo litaanza rasmi
katika mkoa wa Njombe na baadae kufuatia katika mikoa mengine ya
Tanzania hivi sasa linatarajiwa kuanza tarehe 23 ya mwezi huu badala ya
tarehe 16 kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi nchini humo amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuvipa
fursa vyama vya kisiasa kujiandaa na kuandaa watu wake. Hata hivyo,
baadhi ya viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa wamesema kauli hiyo haina
ukweli wowote na kwamba tume inajikosha kwa sababu haina vifaa vya
kutosha vya kuendesha uandikishaji huo. Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau
kutoka Dar es Salaam ametuandalia taarifa ifuatayo:Wakati ikiwa imesalia miezi miwili tu na wiki kadhaa kabla ya tarehe iliyopangwa ya kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, wasi wasi unazidi kutanda miongoni mwa viongozi mbali mbali wa vyama vya kisiasa hapa nchini Tanzania, iwapo Tume ya Uchaguzi nchini humu itaweza kuboresha daftari la wapiga kura katika kipindi cha muda mfupi uliobakia. Baadhi ya viongozi hao wamesema kwamba licha ya tume hiyo kutovishirikisha vyama vya kisiasa katika baadhi ya maamuzi yake, lakini pia wamebaini kwamba mpaka sasa tume hiyo inakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya uandikishaji kwa sababu havijaingia nchini kama ambavyo anabaini Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema.
0 comments:
Post a Comment