
Jeshi la Nigeria limesema kuwa
limewauwa zaidi ya wapiganaji 300 wa Boko Haram, baada ya jeshi la nchi
hiyo kutwaa tena miji kadhaa iliyotekwa na wapiganaji hao kazkazini
mashariki mwa Monguno.
Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.
Bado hakujatolewa taarifa zaidi kuthibitisha habari hizo.
Mataifa
kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon,
ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa
kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Siku
ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji
wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi
uliopita.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment