TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Waziri mkuu Ugiriki ataka aungwe mkono

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema ameliomba bunge la nchi hiyo siku ya Ijumaa kupiga kura ya kuunga mkono mipango yake ya kumaliza masharti yaliyowekwa kwa nchi yake katika kunusuru uchumi wa taifa hiyo.http://www.dw.de/image/0,,18248780_303,00.jpg
Hiyo ni siku ambayo nchi zinazotumia sarafu ya euro zimeweka kama siku ya mwisho kwa Ugiriki kutia saini mkataba unaoipa muda zaidi wa kulipa madeni yake kwa kutakiwa kuheshimu taratibu za matumizi ya fedha.
Hata hivyo maafisa wa Ugiriki wameripotiwa kutaka kuupa Umoja wa Ulaya kuongeza mkataba wa mkopo wake, kama si mpango mzima wa kunusuru uchumi wa nchi hiyo. Habari zinasema bado haijafahamika kama mvutano huu utakubaliwa na EU, ambayo imeiambia Ugiriki kutakiwa kuheshimu makubaliano ya nyuma.
Hadi hapo makubaliano yatakapofikiwa kufikia mwishoni mwa wiki, Ugiriki haitakuwa na fedha. Benki za Ugiriki zinasemekana kuwa na kiwango kidogo cha amana na zimeomba fedha za dharura. Benki Kuu ya Ulaya itaamua Jumatano iwapo iendelee kutoa msaada wa fedha kwa Ugiriki au la.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)