Ameongeza kuwa taifa la Libya halina
uwezo thabiti wa kukabiliana na changamoto inayotolewa na ugaidi,
akitaja haja ya kuzingatia ombi la nchi jirani za Libya la kupatiwa
msaada wa kimataifa. Leonamesema ni muhimu kwa jamii ya kimataifa
kusaidia juhudi za Libya za kukabiliana na ugaidi.Mwakilishi huyo wa
Umoja wa Mataifa amesema timu za mazungumzo zitaanza kukutana leo nchini
Morocco, ili kuridhia ajenda ya awamu ijayo ya mazungumzo yenye lengo
ya kurejesha amani na utulivu nchini Libya. Katika kikao hicho, Balozi
wa Libya katika Umoja wa Mataifa Ibrahim Dabbashi ametoa wito kwa Baraza
la Usalama kuondoa vikwazo dhidi ya nchi yake ili iweze kununua silaha
za kukabiliana na magaidi wa kitakfiri wa Daesh.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment