Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw Meck
Sadik amesema kati ya waliofariki ni watoto wawili na mzee mmoja, ambao
walisombwa na mafuriko.
Amesema kwa sasa serikali inafanya
tathmini kuhusu hasara iliyosababishwa na mafuriko hayo, lakini ripoti
ya awali inaonesha kuwa zaidi ya nyumba 38 katika eneo la Kigamboni
ziliathiriwa vibaya na mafuriko.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ya
Tanzania Bibi Agnes Kijazi amesema mvua hizo ni za msimu. Ameongeza
kuwa mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuwa “hali ya mvua inatarajiwa
kuendelea katika baadhi ya siku hadi Mei 20, mwaka huu”. Mikoa ya Tanga,
Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, pamoja na visiwa vya Unguja na
Pemba pia vinatarajiwa kuwa na mvua kali.
0 comments:
Post a Comment