TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Liverpool, Tottenham zafungasha Europa

http://www.rantsports.com/soccer/files/2014/09/Liverpool-FC-2014-15-EPL-Champions.jpgTimu za Liverpool na Tottenham Hotspur za England jana zilifungasha virago rasmi kwenye mashindano ya ligi ya Europa baada ya kukubali vichapo kutoka kwa wapinzani wao.
Liverpool wakiwa ugenini walikwaana na Besiktas ya Uturuki na kuondolewa kwa mikwaju ya penalti 5 kwa 4 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa sare ya jumla ya goli moja kwa moja na hata baada ya kuongozewa dakika 30 hakupatina mshindi.
Mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye alirudi tena England Demba Ba alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Besitkas waliofunga penalti.
Nayo Tottenham imeondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kupata kichapo cha magoli 2 -0 kutoka kwa Fiorentina na hivyo kuondolewa kwa jumla ya magoli 3 - 1.
Wakati Tottenham na Liverpool zikiondolewa na kwenye michuano hiyo Everton yenyewe imesonga mbele katika hatua ya kumi na sita bora baada ya kuifunga BSC Young Boys ya Uswis kwa jumla magoli 3 -1.
Matokeo mengine Inter Milan ya Italia imesonga mbele baada ya kuifunga Celtic 1 - 0.
Zenit St Petersburg ya Urusi nayo imesonga mbele baada ya kuifunga PSV Eindhoven kwa magoli 3 kwa 0.
Matokeo ya mengine ya mechi za Europa ligi zilizochezwa haya hapa chini
Besiktas 1 - 0 Liverpool (agg 1 - 1)
Fiorentina 2 - 0 Tottenham (agg 3 - 1)
Inter Milan 1 - 0 Celtic (agg 4 - 3)
Everton 3 - 1 BSC Young Boys (agg 7 - 2)
Feyenoord 1 - 2 Roma (agg 2 - 3)
Dinamo Moscow 3 - 1 Anderlecht (agg 3 - 1)
Zenit St P 3 - 0 PSV
Borussia Mönchengladbach 2 - 3 Sevilla (agg 2 - 4)
Dynamo Kiev 3 - 1 Guingamp (agg 4 - 3)
FC Red Bull Salzburg 1 - 3 Villarreal (agg 2 - 5)
Legia Warsaw 0 - 3 Ajax (agg 0 - 4)
Ath Bilbao 2 - 3 Torino (agg 4 - 5)
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)