
Muingereza mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Juba nchini Sudan Kusini.
Makao makuu ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni yamethibitisha kuwa tukio hilo lilifanyika jana jioni katika mji mkuu Juba.
Chanzo cha mauaji hayo hakijulikani.
Mwathiriwa alikuwa akilifanyia kazi shirika moja la kupigania haki za binaadamu la Marekani-Carter Center.
Msemaji
wa serikali Ateny Wek Ateny amesema kuwa mtu aliyejihami na bunduki
alimfuata hadi katika eneo la shirika hilo na kumpiga risasi kabla ya
mtu huyo kutoroka.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment