Wageni hawatoruhusiwa kumiliki ardhi Afrika Kusini, kufuatana na sheria kali zinazopendekezwa na Rais Jacob Zuma.
Siku zijazo wageni wataruhusiwa tu kukodi kwa muda mrefu ardhi ya mashamba ya Afrika Kusini.Mbali ya hayo, mtu yeyote anayemiliki zaidi ya hekta 12,000 atalazimishwa kuiuzia serikali ili ipate kugawiwa.
Tangu kumalizika ubaguzi wa rangi mwaka 1994, chama tawala cha ANC, kimeshindwa kufikia lengo lake la kugawa thuluthi ya ardhi ya kilimo kwa Waafrika, ulipofika mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment