Rais Abdul Fattah al Sisi wa Misri amemfukuza kazi Waziri wa Mambo ya
Ndani Mohamed Ibrahim na badala yake amemteua Magdi Abdul Ghaffar kujaza
nafasi hiyo. Meja Jenerali Magdi Abdul Ghaffar alikuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Usalama wa Taifa ya Misri. Kufutwa kazi Waziri wa Mambo ya
Ndani wa Misri ni katika sehemu ya mabadiliko ya baraza la mawaziri la
nchi hiyo yaliyozijumuisha wizara nane, miongoni mwao ni pamoja na
wizara za elimu, afya, kilimo, utalii na utamaduni. Waziri huyo
aliyefutwa kazi ambaye awali aliteuliwa wakati kulipofanyika marekebisho
katika baraza la mawaziri la Misri mwezi Januari mwaka juzi, amekuwa
akikosolewa vikali kwa nafasi yake kuu katika kuwakandamiza wapinzani.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri aliyefutwa kazi na Rais al Sisi
alikuwa mmoja wa mawaziri wachache walioweza kuhifadhi nyadhifa zao
baada ya Mohamed Morsi, Rais halali wa nchi hiyo kupinduliwa na jeshi
mwezi Julai mwaka juzi.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment