Tanzania imepaa kwenye viwango vya kila mwezi vya FIFA kwa
kupanda kwa nafasi saba (7) katika viwango vya shirikisho hilo la
kimataifa. Rwanda ndiyo imetia fora kwa kupanda kwa nafasi nane (8) na
kuongoza Afrika Mashariki ikiwa nafasi ya 64 duniani ikifuatwa na Uganda
(74), Tanzania, Kenya (118) na Burundi (126). Algeria wanaendelea
kushikilia usukani Afrika wakifuatwa na Ivory Coast, Ghana, Tunisia,
Senegal, Cape Verde, Nigeria, Guinea, Congo DR na Cameroon
wanaokamilisha 10 bora barani. 10 bora duniani inaendelea kuongozwa na
Ujerumani wanaofuatwa na Argentina, Colombia, Ubelgiji, Uholanzi,
Brazil, Ureno, Ufaransa, Uruguay na Italia waliopanda kwa nafasi mbili
na kuitoa Uhispania.
0 comments:
Post a Comment