Idadi ya wahanga wa ugonjwa hatari wa Ebola imepindukia elfu 10. Taarifa
iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) jana usiku, imesema kuwa
idadi ya watu waliopoteza maisha kwa homa ya ugonjwa huo sasa imefikia
watu 10004. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, jumla ya watu walioambukizwa
maradhi hayo katika nchi za Guinea Conakry, Sierra Leone na Liberia
imefikia watu 24,350. Nchi zingine sita zimeripotiwa kupata maambukizi
ya ugonjwa huo kwa kusajiliwa visa 15 vya maradhi hayo. Kesi ya kwanza
ya maambukizi ya maradhi ya Ebola iliripotiwa mwezi Januari mwaka jana
2014 nchini Guiena Conakry. Wataalamu wa Benki ya Dunia, wametaja hasara
inayokaribia dola bilioni moja na milioni 600 za Marekani
iliyosababishwa na maradhi hayo. Mwanzoni mwa mwezi huu Shirika la Afya
Duniani (WHO) lilitangaza kuanza majaribio ya kwanza ya chanjo ya homa
ya Ebola kwa kiwango kipana zaidi nchini Guinea Conakry.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment