Katika kikao hicho, Kiongozi Muadhamu aliashiria masuala ya
sasa katika eneo na changamoto zilizojitokeza kutokana na sera za
undumakuwili za nchi za Magharibi. Katika sehemu ya hotuba yake,
sambamba na kubainisha sera za kistratijia za Iran katika mazungumzo ya
nyuklia, aliashiria pia barua ya hivi karibuni ya maseneta wa Marekani
na kusema hiyo ni ishara ya kusambaratika maadili ya kisiasa katika
mfumo wa Marekani.
Kiongozi Muadhamu aliongeza kuwa kila wakati unapokaribia
muda ulioainishwa kumalizika mazungumzo ya nyuklia, matamshi ya upande
wa pili hasa Marekani huwa makali na ya kijeuri zaidi na hii ni sehemu
ya ujanja na hila zao. Amesema mbinu hii ni ya kujaribu kukwepa uhalisia
wa mambo na kwamba haina faida yoyote ila kufichua njama za Marekani na
utawala wa Kizayuni wa Israel ambao ndio mmiliki pekee wa silaha hatari
za nyuklia katika Mashariki ya Kati.
Jitihada za hivi karibuni za Wazayuni, na hasa Waziri Mkuu
wa Utawala wa Kizayuni ambaye alitoa hotuba isiyo na maana katika Bunge
la Kongresi Marekani, ni sehemu ya silisila ya njama za Marekani za
kutafuta vizingizio ili kukwepa kutekeleza majukumu yake kimataifa. Kama
alivosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, hatua ya
Netanyahu ambaye ni kikaragosi cha Uzayuni kufika katika Kongresi na
kutoa hotuba duni na baada ya hapo baadhi ya wajumbe wa Kongress
kuandika barua inayohusiana na hotuba hiyo, ni siasa zisizo na maana.
Watawala hao wa Marekani na Israel ambao ndio waungaji
mkono asili wa magaidi kwa mara kadhaa wameituhumu Iran kuwa inahusika
na ugaidi lakini uzoefu umeonyesha kuwa matamshi kama hayo na barua kama
hizo haziwezi kubadilisha ukweli wa mambo.
Kama ambavyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran Mohammad Javad Zarif alivosema, katika kujibu barua ya Maseneta
wa Marekani, 'hao maseneta wanapaswa kufahamu kuwa, dunia si Marekani,
na kanuni za mahusiano baina ya nchi zinafuata sheria za kimataifa si
sheria za ndani za Marekani.'
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kikao na
wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu alisisitiza kuhusu nukta mbili
muhimu. Awali ni kuwa Iran inatekekeza sera za uwazi na ukweli katika
mazungumzo ya nyuklia na pia timu ya wanadiplomasia wa Iran katika
mazungumzo hayo wanafuata sera hizo. Pamoja na hayo kuna shaka kuhusu
mwenendo wa upande wa pili katika mazungumzo. Kama alivyosema Kiongozi
Muadhamu, upande wa pili katika mazungumzo ya nyuklia ni hodari kwa
kufanya hila, ujanja na usaliti.
Nukta ya pili ni kubainisha utumbulisho uliojaa hadaa wa
utawala wa Kizayuni na himaya ya wazi na daima ya mrengo wa wenye
misimamo mikali Marekani kwa utawala huu utendao jinai. Lakini hivi sasa
utumizi wa mbinu hizo umefika ukingoni. Pamoja na hayo, watu
wanaofungamana na mrengo wa Uzayuni katika Kongresi ya Marekani
wanajaribu kuibua kelele kwa kisingizio cha kuzuia kile wanachosema kuwa
ni 'mkataba mbaya wa nyuklia na Iran. Lengo la Wazayuni na waitifaki
wao katika Kongresi ya Marekani ni kupotosha fikra za waliowengi
duniani.
0 comments:
Post a Comment