TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Al-Shabab wamteka nyara kiongozi wa serikali Kenya

Al-Shabab wamteka nyara kiongozi wa serikali KenyaDuru za habari nchini Kenya zimeripoti taarifa ya kutekwa nyara kiongozi mmoja wa serikali ya nchi hiyo na kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab la nchini Somalia. Mukhtar Maalim Adan, ambaye ni afisa utawala katika mji wa Mandera nchini Kenya, ametekwa nyara na kundi hilo ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara nchini humo. Maafisa wa polisi wamesema kuwa, Mukhtar ametekwa nyara alipokuwa safarini kutoka mjini Mandera kuelekea moja ya miji ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambapo alivamiwa na wanachama wa kundi hilo na kisha kuchukuliwa kwa gari lake na kupelekwa kusikojulikana. Hadi sasa polisi bado haijafanikiwa kunasa gari ya Mukhtar Adan na ingali inaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika wa tukio hilo. Hata hivyo polisi ya Kenya ina wasi wasi kwamba huwenda kiongozi huyo wa serikali akawa amepelekwa Somalia na kundi hilo la kigaidi. Mji wa Mandera uko katika mpaka wa pamoja wa Kenya na Somalia ambapo unatajwa kuwa njia mojawapo muhimu inayotumiwa na wanachama wa ash-Shabab kuingilia nchini Kenya na kutekeleza uhalifu wao. Licha ya kwamba hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na tukio hilo la utekaji nyara, lakini kidole cha lawama kimeelekezwa kwa kundi hilo ambalo wiki kadhaa zilizopita, lilitekeleza hujuma kali dhidi ya Chuo Kikuu cha mji wa Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya na kuua watu 150 wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)