Timu ya Chelsea imeibuka mabingwa wa
ligi kuu ya England, baada ya kuifunga Crystal Palace bao 1-0 katika
mchezo uliofanyika katika uwanja wa Stamford Bridge. Bao la Chelsea
lilifungwa katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza cha mchezo,
likifungwa Eden Hazard.Chelsea ilihitaji pointi tatu kutangazwa
mabingwa wa ligi kuu ya England. Chelsea imetwaa ubingwa huo ikiwa bado
na michezo mitatu, ikiwa imejikusanyia pointi 83 ikifuatiwa na mabingwa
wa msimu uliopita Manchester City yenye pointi 70, huku Arsenal ikiwa
katika nafasi ya tatu na pointi 67 na nafasi ya nne inakaliwa na
Manchester United yenye pointi 65.
Karibu timu zote za ligi hiyo ikiwa ni pamoja na nne za juu zimecheza michezo 35, isipokuwa Arsenal yenye michezo 33.
Jose Mourinho, kocha wa Chelsea
Ubingwa huo umemfanya kocha wa
Chelsea Jose Mourinho ajisikie furaha, ajivune na kujisikia mchovu baada
ya kazi ngumu ya kusaka taji hilo.
Ushindi huo umempa Mourinho
ubingwa mara tatu akiwa kocha wa Chelsea, na kombe lake la kwanza akiwa
kocha wa Chelsea mara baada ya kurejea mara ya pili kukiongoza kikosi
hicho smimu uliopita. Hili ni taji la tano kwa klabu hiyo na limekuja
miaka mitano baada ya timu hiyo kuchukua kombe lake la mwisho na ni
miaka 60 tangu wachukue kombe la kwanza.
Shangwe na shamra shamra
zilitanda kuzunguka eneo la Stamford Bridge baada ya filimbi ya mwisho
kupulizwa. Kwa hakika Chelsea ilistahili kutwaa kombe hili kutokana kasi
waliyoweka tangu kuanza kwa msimu wa ligi hiyo.
Ligi ikielekea
ukingoni timu za Sunderland, QPR na Burnley ndizo ziko katika hatari
zaidi ya kureremka daraja. Hata hivyo hali si shwari pia kwa timu za
Leicester, Hull, Newscastle na Aston Villa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment