TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Israel yafanya mashambulizi ya anga nchini Sudan

Israel yafanya mashambulizi ya anga nchini Sudan  Gazeti moja la Kizayuni limearifu kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya mashambulizi ya anga huko Sudan. Gazeti la Kizayuni la Maariv limezinukuu duru za Sudan na kuandika kuwa, ndege za Israel kwa mara nyingine tena zimeishambulia Sudan. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, duru za Sudan zimetangaza kuwa sauti za milipuko zilisikika jana usiku huko Khartoum mji mkuu wa nchi hiyo kufuatia mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Baadhi ya duru za Kiarabu pia zimetangaza kuwa mashambulizi hayo yalikusudiwa kukilenga kituo kimoja cha kuundia silaha. Wakati huo huo viongozi wa Sudan wameashiria rekodi ya mashambulizi ya huko nyuma ya Israel dhidi ya nchi hiyo na kuunyooshea kidole cha tuhuma moja kwa moja utawala huo ghasibu.

Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)