Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, sehemu kubwa ya maeneo ya
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, yamekombolewa kutoka mikononi mwa
wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram. Jeshi la nchi
hiyo limetangaza kuwa, operesheni pana zilizotekelezwa katika maeneo ya
mpakani ya Madagali karibu na jimbo la Borno, kaskazini mwa Nigeria
sasa yamekombolewa kutoka kwa wanamgambo hao. Akizungumza Jumatano
iliyopita, Rais Good Luck Jonathan wa nchi hiyo alisema kuwa majimbo
mawili ya Adamawa na Yobe nayo yatakombolewa wiki chache zilizosalia
kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram. Alitabiri kuwa, hadi wiki tatu
zijazo jimbo la Borno pia litakuwa limesafishwa kabisa kutokana na uepo
wa wanachama wa kundi hilo linalofahamika kwa kutenda jinai dhidi ya
binaadamu nchini humo na nchi jirani. Weledi wa mambo wanazitaja
operesheni za majeshi ya muungano wa nchi jirani kwa kushirikiana na
jeshi la Nigeria kuwa ni njama za kumsafishia njia kuelekea ushindi
katika uchaguzi mkuu ujao nchini Nigeria, Rais Jonathan hasa kwa
kuzingatia kuwa, kumekuwepo na tetesi kwamba kiongozi huyo ana
ushirikiano na kiongozi mkuu wa kundi hilo la kitakfiri na lenye uelewa
potofu wa dini ya Kiislamu, Abubakar Shekau.
0 comments:
Post a Comment