
Kushadidi kwa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel kumekabiliwa
na radiamali mbalimbali za kimataifa. Umoja wa Ulaya (EU) umelaani
hatua ya utawala haramu wa Israel ya kubomoa nyumba za Wapalestina
katika maeneo ya Quds inayokaliwa kwa mabavu. Taarifa ya umoja huo
imelaani kubomolewa nyumba za Wapalestina huko Baitul Muqaddas Mashariki
na kuitaka Israel ikomeshe vitendo vyake hivyo. Nyumba hizo zipatazo
200 zilikuwa zimejengwa kwa msaada wa fedha uliotolewa na Umoja wa
Ulaya. Hivi karibuni, Utawala wa Kizayuni umeshadidisha mashinikizo
dhidi ya Wapalestina wanaoishi kwenye maeneo yaliyoanza kukaliwa kwa
mabavu na utawala huo ghasibu mwaka 1948. Uporaji wa ardhi, kuwatoa watu
majumbani mwao, kubomoa nyumba zao na kupitisha sheria mpya za kibaguzi
dhidi ya Wapalestina ni sehemu tu ya hatua zisizo za ubinadamu
zinazowanyima Wapalestina hao haki za kijamii na kiuchumi. Radiamali
nyengine dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni imetolewa na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Nchi za Kiislamu
(ISESCO). Abdulaziz bin Othman At-Tawijri amesema Israel ni nembo ya
ugaidi na kuongeza kwamba vitendo vya utawala wa Kizayuni dhidi ya
Wapalestina vikiwemo vya uvamizi na ukaliaji wa mabavu, ubomoaji,
mauaji, ukandamizaji n.k. vina sura na utambulisho kamili wa kigaidi, na
vinakinzana na sheria na hati za kimataifa. Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO
amesisitiza kwamba kukabiliana na vitendo hivyo vya kinyama vya utawala
haramu wa Israel si jukumu la nchi moja maalumu au majimui ya nchi
fulani tu bali ni wajibu wa Jamii ya Kimataifa; na uzembe au ajizi
yoyote inayofanywa juu ya kukabiliana na ugaidi huo wa kiserikali ina
matokeo mabaya yanayotishia amani na usalama wa dunia. Wakati huohuo
Kundi la Kiarabu la Ustawi wa Kitaifa lenye makao yake mjini Geneva
limekosoa vikali kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kutokabidhi
viwiliwili vya mamia ya Wapalestina kwa familia zao. Taarifa iliyotolewa
siku ya Jumatano na kundi hilo imeeleza kuwa viwiliwili vya watu hao
vimezikwa kwa siri kwenye maeneo ya kijeshi ya ardhi za Palestina
zilizoanza kukaliwa kwa mabavu mwaka 1948, na hakuna mwenye haki ya
kuyakaribia makaburi yao. Kundi la Kiarabu la Ustawi wa Kitaifa
limebainisha kwamba katika ulimwengu mzima ni utawala wa Kizayuni pekee
ndio ulioweza kufanya vitendo viovu kama hivyo katika kuamiliana na
Wapalestina na Waarabu, kwani hata baada ya Wapalestina hao kuuawa
shahidi utawala huo khabithi unaziadhibu familia zao kwa kuwanyima haki
ya kuwazika watu wao mahali wanapotaka kwa mujibu wa sheria za dini.
Kundi hilo limesisitiza kwamba kitendo hicho cha utawala wa Kizayuni ni
jinai ya kidini, kisheria na kimaadili na ni ukiukaji wa wazi wa sheria
za kimataifa zinazohusiana na haki za binadamu pamoja na Mkataba wa Nne
wa Geneva. Kundi la Kiarabu la Ustawi wa Kitaifa limetoa wito kwa
jumuiya za kimataifa ziushinikize utawala wa Kizayuni uvikabidhi
viwiliwili vya mashahidi hao wa Kipalestina kwa familia zao. Hii ni
katika hali ambayo Makarim Wibisono, ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa
wa hali ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa
mabavu ameeleza katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusiana na jinai
zilizofanywa na utawala wa Kizayuni mwaka uliopita wa 2014 za mauaji ya
zaidi ya Wapalestina 2,000 wakati wa vita vya siku 50 dhidi ya Ukanda wa
Gaza, kwamba theluthi moja kati ya waliouawa walikuwa ni watoto
wadogo…/
0 comments:
Post a Comment