Kwa mujibu wa ripoti moja, kwa sasa wapiganaji mia moja na hamsini wa kundi la Islamic State wameendelea kuwepo katika mji huo wa Tikrit, ambao ni makao makuu ya jimbo la Salahuddin.
Mkuu wa operesheni za kijeshi katika jimbo hilo Luteni Jenerali Abdul-Wahab al Saadi amesema operesheni hiyo itaendelea mpaka wapiganaji hao wa Islamic State watakapoondolewa.
''...Mapambano kuusafisha mji wa Tikrit yanaendelea, tumeanzisha operesheni kadhaa za kijeshi- kiasi cha operesheni tano au sita hivi.
Wakati huu tunapozungumza operesheni za kijeshi zinaendelea na zitaendelea mpaka tutakapolikomboa jimbo zima la Salahuddin. Mungu akipenda...''
Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Baghdad, Waziri mkuu wa Iraq, Haider al Abadi, ameelezea kufurahishwa kwake kutokana na majeshi ya nchi hiyo kuendelea kupata ushindi dhidi ya wapiganaji hao wa Islamic State, mjini Tikrit.
Ushindi mkubwa tulioupata ni kuunganisha nchi, umoja kwa ajili ya kuushinda ugaidi katika ardhi ya Iraq, kuwashinda wote wanaotaka kuwadhuru watoto wetu, nchi yetu na watu wetu. Huu ni ushindi halisi tulioupata leo...''.
0 comments:
Post a Comment