TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Mgombea Urais mwanajeshi hatakiwi Burkina Faso

Mgombea Urais mwanajeshi hatakiwi Burkina Fasoumuiya za kiraia za nchini Burkina Faso zimetangaza kuwa zinapinga kushirii wanajeshi katika uwanja wa siasa nchini humo. Jumuiya hizo zenye mfungamano na makundi ya kiraia ya Burkina Faso zimetoa taarifa na kumtaka Rais wa mpito wa nchi hiyo mwanadiplomasia Michel Kafando azuie kurejea katika uwanja wa siasa nchini humo Blaise Compaore rais wa  nchi hiyo aliyelazimika kujiuzulu kufuatia mashinikizo ya wananchi.
Jumuiya za kiraia za Burkina Faso zinaamini kuwa, Compaore ambaye sasa anaishi nchini Ivory Coast, anafanya kila analoweza ili kushiriki tena katika masuala ya siasa za Burkina Faso. Wakati huo huo jumuiya za kiraia za nchini Burkina Faso zimeitaka serikali ya muda ya nchi hiyo azuie wanajeshi kushiriki kama wagombea katika uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu ili uchaguzi huo ufanyike vyema pasina mivutano yoyote. Wagombea wengi wanaotarajiwa kushiriki katika uchaguzi ujao wa Rais wa Burkina Faso ni wanajeshi.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)